Mwezi wa kumi mwaka huu nilikwenda pamoja na watu tisa wengine kwenda Marangu. Katika Marangu tulitaka kuangalia na kucheki miradi iliyoanza kabla ya safari hii mwaka uliopita na pia kuanza miradi tofauti. Sisi tumetoka Hamburg, Ujerumani. Hapo tunafanya kazi kwa shirika linaloitwa „Marangu e.V“.

Shirika hili linasaidia miradi tofauti mingi katika mkoa wa Marangu/ Kilimanjaro.

Mradi mmoja wa shirika yetu ni  “Mradi wa mbuzi na kuku kwa wanawake, wanaogonjwa wa ukimwi“.  Kwa hivyo safari yetu tuliwatembelea wanawake ishirini, waliopata zizi la mbuzi au zizi la kuku na wanyama hawa pia.  Mazizi yote waliolipwa kwa shirika „Marangu e.V“.

Pale hali ya mkoa ni mbaya sana, kwa sababu hakuna mvua tangu mwaka 2010. Kwa hivyo kuna vumbi nyingi.  Tunafurahi sana kusaidia wanawake hawa, wanoisha mkoa huu bila maji.

Mama Shayo na Mama Nyau, wanaoangalia mradi wa „Home-care“, na bibi Aripa anafanya kazi chama cha MACDA. Wanawake watatu wameuangalia na wameumaliza mradi wa mbuzi na kuku huu pia. Wanawake watatu wamefanya kazi nzuri sana!  Kwa sababu kuna masharti magumu, kwa mfano hakuna ruhusa kukata miti katika mkoa wa Kilimajaro, kwa hivyo miti iliipatwa kutoka mikoa mingine, iko mbali sana.

Safari yetu tuliona, kwamba mbuzi na kuku wamezaa na sasa kuna watoto wadogo wa mbuzi na kuku pia.

Mbuzi yenye kwa nguvu. Kwa hivyo wanaweza kulisha watoto wao na pia maziwa yao yanatosha kununua sokoni. Jogoo na kuku yenye nguvu sana pia. Kwa sababu kuna mayai mingi, wanawake wanaweza kununua mayai na kufanya biashara.

Tunafurahi sana kusaidia wanawake wengi na mradi hii na pia tunafurahi, kwamba Mama Shayo, Mama Nyao na Aripa wamefanya kazi nzuri nzuri sana.

Asante sana, Mama Shayo, Mama Nyau na Aripa!

Wasalaam,

Hans-Jürgen Buhre

©2012 Förderverein Marangu e.V.